GET /api/v0.1/hansard/entries/1374164/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1374164,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1374164/?format=api",
    "text_counter": 245,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika. Kwanza ni kutoa kongole kwa Kamati hii ya Kitaifa kwa sababu ya mazungumzo yaliyofanyika baina ya pande zote mbili; Upinzani na wale wa Serikali. Ripoti hii inaashiria maoni kutoka kwa Wakenya kwani wengi waliichangia. Si kazi rahisi baada ya uchaguzi, watu kuketi kutoka pande zote mbili na kukubaliana jinsi ya kuendeleza nchi yao. Jambo ambalo liliwekwa kipaumbele ni uhamiaji wa wanasiasa kutoka kwenye vyama vyao na kuenda katika vyama vingine. Hili jambo limekuwa likitendeka sana kwenye siasa. Wanasiasa wanakimbilia vyama fulani, alafu baadaye wanaondoka na kuenda vyama vingine. Makubaliano haya ni ya muhimu sana. Wakenya walikubaliana kwamba hili jambo liwekwe kwenye sheria, ambapo ukihama chama kilichokuchagua, utapoteza kiti chako cha wale wananchi waliokuchagulia na kukuleta Bungeni. Pendekezo hili ni muhimu sana, na inafaa liingie kwenye Katiba kuzuia wale wazembe wa siasa. Kutokana na mazungumzo yale, pendekezo kwenye Ripoti hii ni sheria iangaliwe ili iweke Bunge la Seneti kama nyumba ya juu. Maseneta wanaweza kukaa kwa muda wa miaka saba hapa Seneti. Hili ni jambo ambalo litaleta mwamko mpya. Seneta ambaye ana constituencies mingi katika kaunti yake utapata kwamba kazi yake huwa nyingi zaidi. Kwa hivyo, ukipewa kama miaka saba, nafikiria ndio sawa kwa sababu ukiwa na kaunti kubwa unaweza kuzunguka na hatimaye ukaweza kufika kila mahali. Mimi ninasema hivyo kwa sababu niko na experience . Kwa ile miaka mitano ya kwanza, utakuwa unajidanganya ukisema ya kwamba utaenda kila mahali wewe kama Seneta ili uweze kupatikana kule. Kawaida huwa unaweza kwenda, ukafika mahali na ukaona kwingine unapeleka pengine zile picha zako za campaign pekee yake, ukisema kwamba kule huwezi kufika kwa sababu kaunti zinakuwa ni kubwa zaidi. Kwa hivyo, nafikiria wakipewa hii miaka saba alafu pengine tena ukaruhusiwa kurudi usimame tena, nafikiria itakuwa ni jambo nzuri kwa sababu, zile kazi wanazofanya ziko tofauti ikilinganishwa na wale ambao wanachaguliwa kama wawakilishi wa Bunge la Kitaifa. Mimi ninaona ni jambo nzuri kuona ya kwamba, hivi sasa Maseneta wanaweza kupewa nafasi ya kuweza kufanya kazi yao ndani ya Bunge kwa miaka saba. Bw. Spika, tunaona ya kwamba pia vile vile katika mazungumzo haya yaliweza kutoa siku 14 zile ambazo watu wanaweza kuenda mahakamani; hususan tukiona ya kwamba mara nyingi ni sisi watu wa upinzani ndio tumekuwa tukienda mahakamani tukitaka haki zetu kwa sababu tumeibiwa kura. Bw. Spika, naona siku 14 zile ambazo mawakili wanapewa nafasi ya kuweza kutayarisha makaratasi yao, baadhi kuyapeleka mahakamani na pia kesi kusikizwa, katika hiyo muda uliopewa, mimi kwa maoni yangu nikiwa kama mmoja wa wale watu walikuwa wanaketi kusikiza kesi za watu, naona ya kwamba siku 14 ni ukweli kabisa kwamba ni kidogo."
}