GET /api/v0.1/hansard/entries/1374166/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1374166,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1374166/?format=api",
"text_counter": 247,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Kwa hivyo, zile siku 21 ambazo zimepeanwa ili mawakili na korti ziweze kutafakari ama kuangalia ile kesi na hatimaye kuamua kesi ambayo itakuwa ni ile ya Raisi, tunaona kwamba hii itakuwa ni vyema zaidi. Bw. Spika, nataka pia kuwapatia kongole zaidi kwa ule muda na wakati ambao wale ambao tulikuwa tumewapatia nafasi hii, ilikuwa si kazi rahisi. Waliweza kusaidia hii nchi. Waliweza kutuokoa sisi katika vile vita ambavyo vilikuwa vinaweza kutokea ama vilitokea na baada ya hapo tukapata amani. Kwa hivyo, kuja na taarifa kama hii, katika kamati hii iliyoketi katika mazungumzo, nataka kuwapa kongole zaidi sana. Mwenyezi Mungu tunajua anaweza kupeleka hii nchi yetu mbele kisawasawa na amani. Asante."
}