GET /api/v0.1/hansard/entries/1375549/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1375549,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1375549/?format=api",
    "text_counter": 417,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa nami nitoe sauti yangu kuhusu Ripoti hii ya uwiano ambayo imetolewa. Kwanza, ninapongeza wenzangu. Nimeona wengi walitoa matakwa mengi kuhusu pesa zinazofaa kuelekezwa kwa MCAs wetu. Ni dhahiri kuwa MCAs wetu wamekuwa wakihangaika sana. Wengine wanapewa pesa; wengine hawapewi. Itasaidia sana kukiwekwa sheria kuwa MCAs wapewe pesa za kufanya miradi kule mashinani. Jambo lingine ambalo nitaliangazia ni la walemavu, ijapokuwa sijui kama litapewa kipaumbele. Sikuliona katika yale maamuzi ya mwisho. Walemavu siku zote huwa wameachwa nyuma na ingekuwa vizuri kama wangekuwa na mgao wao wenyewe ambao utawawezesha kupanga mambo yao bila kushughulisha watu wengine tofauti. Walemavu wanahangaika kwa mambo mengi sana katika taifa hili na wanahitaji usaidizi. Ikiwa watatengewa mgao wao, itawasaidia sana. Jambo lingine lililogusiwa ni la IEBC. Katika uchaguzi uliopita, tuliona mambo yalivyokuwa. Ilionekana wazi kuwa uzito wa makamishna wanne unashinda wa makamishna watatu. Wakati huo ilikuwa vigumu sana kuelewa vipi uzito wa makamishna watatu unashinda wa wanne. Ikiwa mambo hayo yanaweza kuangaliwa vizuri na yapigwe msasa, tutajua makamishna wa IEBC wanapewa uzito gani ili tuelewe ni kwa sababu gani wale makamishna watatu walipewa uzito mkubwa kuliko wale wanne. Jambo hili lipigwe msasa ili mambo haya yasirejelewe. Jambo lingine ni la sheria ya thuluthi mbili kuhusu jinsia. Ningependa akina mama wa Bunge hili tulisukume kwa pamoja. Hata dada yetu Waziri, Mhe. Aisha Jumwa, alisukume kwa haraka jambo hili la sheria ya thuluthi mbili kuhusu jinsia. Akina mama wanahitaji nafasi za kutosha za uongozi kama inavyo sema Katiba. Ningependa kumweleza Waziri wetu, Aisha Jumwa, ailete sheria hiyo haraka ili iingizwe ndani ili mambo ya akina mama yaangaliwe kisawasawa. Sisi kama viongozi kutoka pwani, tulililia Kamati hii iangalie mipaka yetu ambayo huingiliwa na watu wa sehemu za Garissa na ukambani ili iweze kulindwa. Naona limegusiwa kwenye Ripoti. Ripoti hii ikichukuliwa kwa uzito, sehemu zetu za pwani zitapata ulinzi na tutabaki na amani katika sehemu zetu. Jambo lingine tuliloliomba ni kuwa constituencies tulizonazo zisipunguzwe. Kulikuwa na tetesi kuwa zitapunguzwa. Idadi yetu imeongezeka. Tunaomba kuwa, badala ya kupunguza, waongeze constituencies zingine katika sehemu zetu. Tutashukuru. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}