GET /api/v0.1/hansard/entries/1375550/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1375550,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1375550/?format=api",
    "text_counter": 418,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Wengi wamezungumza na wakasema kuwa, mpaka sasa, gharama ya maisha iko juu sana. Sisi sote ni Wakenya. Tunapozungumza si eti tunachukiana. Tunataka gharama ya maisha irudi chini na mwananchi mnyonge kule chini aweze kukidhi matakwa yake bila uzito. Unga haijashuka bei kama alivyosema mwenzangu. Tusukume wakulima. Mbolea ilikuja bure na wakulima wakauziwa. Wakulima wapewe mbolea bure. Kwa sababu mazao yameongezeka, wakulima wakipewa mbolea bure, mazao yao yatazidi kuongezeka na uchumi wetu utapanda juu. Ninaipongeza Ripoti hii na kama Mama Mombasa, ninasema ni Ripoti nzuri ambayo ikitiliwa maanani tutasonga mbele kama Kenya moja. Asante."
}