GET /api/v0.1/hansard/entries/1375701/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1375701,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1375701/?format=api",
    "text_counter": 135,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii niwakaribishe wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Embu. Wanafunzi hawa wana bahati kwani wamekaa katika Bunge hili la Seneti karibu saa moja. Ni matumaini yangu kuwa wamejifunza mengi. Ili wawe viongozi ama Maseneta wa kesho, ni lazima waache mada za kulevya na pombe. Kama mnavyoona, sisi tuna umoja ijapokuwa kuna Maseneta wa upande wa walio wengi na walio wachache. Huko nje mtaona ni kama kwamba kuna shida kati yetu, lakini sisi tunafanya kazi pamoja. Mkirudi mpeleke salamu za Maseneta wote kutoka Seneti ya Kenya."
}