GET /api/v0.1/hansard/entries/1375724/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1375724,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1375724/?format=api",
    "text_counter": 158,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa fursa hii umenipa ili niunge mkono huu Mswada wa Parliamentary Powers and Privileges ambao umeletwa na Seneta wa Vihiga, Sen. Osotsi. Huu ni Mswada mzuri ambao unapatia uhai Ibara ya 125 ya Katiba. Bunge inaweza ita mtu yeyote ili kuja kutoa ushahidi kuambatana na Ibara ya 50 ambayo inatoa ruhusa kwa mtu yeyote kusikizwa. Bw. Spika, nimekuwa katika Seneti hii kwa muda wa miaka saba. Tumekuwa na shida wakati mwingine kupata watu ambao wanahitajika kuja kutoa ushahidi, hasa magavana ama mawaziri. Hii imepelekea kutopata ukweli kuhusu mambo kadha wa kadha. Seneti iliyopita kuna magavana ambao walikataa kuja mbele ya CPAC kutoa ushahidi. Pesa nyingi sana zimeenda katika magatuzi kwa sabau ya ugatuzi lakini zimefujwa na hazijatoa huduma kwa wananchi wetu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}