GET /api/v0.1/hansard/entries/1375725/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1375725,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1375725/?format=api",
    "text_counter": 159,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Pia kuna Mawaziri wa Serikali ya kitaifa ambao wamehitajika kuja kutoa ushahidi lakini hawaji. Hiyo imepelekea kucheleweshwa kupata majibu ya Petitions nyingi. Nakubaliana kwamba faini ambayo inatolewa ni ya kiwango cha chini sana. Wakati Maseneta wengine walipokuwa wanachangia Mswada huu, walisema baadhi ya magavana huuliza Mpesa ama Paybill namba ili walipe faini hiii ya Kshs500,000. Nifikiri hayo ni madharau. Ninaunga mkono wengine ambao wamechangia na kusema hii faini iongezwe hadi milioni kumi. Pia kuwe na njia ya kuifanya hiyo iwe kama deni ambayo italipwa kuambatana na Public Debt Act. Pia ninaunga mkono kuwe na mbinu ya kuwalazimisha mashahidi kuja mbele ya Seneti au kamati ili kutoa ushahidi. Wasipokuja, basi kuwe na mbinu ya kuwashika na kuwalazimisha kuja mbele ya Bunge na kutoa ushahidi. Ninaunga mkono ikiwa kama inawezekana, kituo cha polisi cha Bunge kipewe nguvu ya kuwashika hawa mashahidi ambao hawataki kuja mbele Bunge kutoa ushahidi. Bw. Spika, kutia nguvu hii sheria itaipatia Bunge meno na uwezo zaidi ambao utawezesha sisi kufanya kazi yetu ya uangalizi ama oversight . Hii ni sababu kazi yetu imekumbwa na changamoto nyingi kwa sababu Bunge linaonekana kama halina meno ama uwezo wa kutosha wa kuleta mashahidi kutoa ushahidi mbele yake. Sina mengi zaidi ya hayo. Mswada wa Sen. Osotsi ni mzuri. Tunatakiwa tuunge mkono kwa sababu unapelekea kufanya rahisi kazi ya Bunge ili kuhakikisha ya kwamba pesa zinazotolewa na wananchi kwa njia ya ushuru, zinafanya kazi vizuri. Hii sheria itafanya sisi kama Wabunge na wawakilishi wa wananchi, tukiitisha"
}