GET /api/v0.1/hansard/entries/1375771/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1375771,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1375771/?format=api",
    "text_counter": 205,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa kukaribisha wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Makima ambao wamekuja kujifunza katika Seneti. Karibuni sana wanafunzi. Mkiwa huko nje, huwa mnasema kwamba hapa hatuelewani kwa sababu kuna upande wa walio wachache na upande huu wa walio wengi. Tukiingia hapa, sisi huwa kitu kimoja. Mtakaporudi nyumbani, muweze kutia bidii masomoni kwa kuwa ninyi ndio viongozi wa kesho. Ili kuwa na maisha mazuri, jiepusheni na pombe, dawa za kulevya na mambo mengine. Mmekuja hapa kujifunza jinsi Seneti inavyofanya kazi na kuhakikisha kuwa pesa zinatumwa katika kaunti zetu. Tunahakikisha kuwa pesa hizo zinatumiwa vizuri. Tunaelewa kuwa mkiwa shuleni, mnahitaji karo, pesa za kulipa maji na gharama zingine. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}