GET /api/v0.1/hansard/entries/1375813/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1375813,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1375813/?format=api",
    "text_counter": 247,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada huu ambao unapendekeza hatua ambazo zita chukuliwa wakati magavana wanapoalikwa kwa Kamati kujibu maswali na wanakosa kuja. Miaka 10 ya ugatuzi imepita. Pesa nyingi zimetumwa kwa makaunti lakini zimetumiwa visivyo na magavana na wafanyikazi wa kaunti. Maseneta wakipendekeza pesa kidogo zigawiwe kaunti, waohulalamika na tunakuwa maadui. Pia tukiwaongeza pesa--- Tunapoenda mashinani kuangalia kazi waliyofanya, wanakataa kutuona hadi kwenye mikutano. Tunapowahitaji wajibu maswali kuhusiana na utumizi wa pesa kwenye Kaunti, inakuwa ni shida na wanatoa vigezo kama vile, kuwa na kazi na shughuli nyingi. Tunafaa tuchukue hatua na kuangalia faini ya kutohudhuria kikao cha Kamati. Kwa mfano, Kshs2 millioni kama inavyopendekezwa kwenye Mswada. Gavana wa Embu anajaribu kufanya kazi. Lakini, miaka 10 ya ugatuzi, pesa ilitumika kwa njia zizofaa. Kaunti ilikuwa na mzozano na vita baina ya viongozi. Gavana aliyechaguliwa kwenye uchaguzi uliopita alipata pesa zimetumika kwa njia ambayo haifai. Mabenki haikuwa inalipwa na hospitali za kaunti kuzoroteka. Naunga mkono faini iliyopendekezwa. Pia, tunafaa tujue hatua tutakayo chukua dhidi ya magavana wa zamani waliotumia pesa za Kaunti vibaya na hakuna hatua imechukuliwa. Naomba tuwe na pendekezo kwenye Mswada, ili tuweze kuchukulia magavana hawa hatua. Naunga mkono Mswada huu ili magavana waweze kufunguliwa mashtaka kortini. Pia tukihitaji magavana kwenye Kamati kuwe na askari maalum wasio wa Serikali wafanya kazi hii. Askari ambao tunafanya kazi nao kwenye Bunge wanafanya kazi nzuri. Kuna siku niliona rafiki yangu, Sen. Cherarkey, akiinuliwa juu na askari. Tunahitaji askari hawa ili walete magavana ambao hawaitiki wito. Asante, Bw. Spika wa Muda. Naunga mkono Mswada huu."
}