GET /api/v0.1/hansard/entries/1375914/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1375914,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1375914/?format=api",
    "text_counter": 48,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Runyenjes, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Muchangi Karemba",
    "speaker": null,
    "content": ", Chifu, Naibu wa Chifu na wazee wa vijini, watu ambao wanaonekana wa kwanza kunapotokea jambo lolote ni wazee wa vijiji. Mara nyingi, utasikia wakipatiwa heshima kubwa sana wakiwa kwa vijiji. Lakini heshima hiyo haiambatani na marupurupu. Kwa muda mrefu, wamekuwa wakitumia pesa zao kununua sabuni na chakula. Wanatumia muda mwingi kwenye mikutano ilhali hawapewi chochote. Wakati uliopita, tuliweza kuzungumzia suala la kuwalipa marupurupu wazee wa vijiji hapa Bungeni, lakini hatujafika mahali pa kuwawezesha kulipwa pesa zao. Naona sheria hii ambayo tunaunda wakati huu itawasaidia ili watambuliwe kisheria na serikali kwa sababu wamekuwa wakijulikana hivi hivi. Tukipitisha sheria hii, Waziri wa Fedha na yule wa Interior and National Administration wataweza kuketi na kujua ni vipi hao wazee muhimu watapata marupurupu yao kwa sababu kwa muda mrefu, wametumia wakati na nguvu zao bila kupata chochote. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}