GET /api/v0.1/hansard/entries/1375924/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1375924,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1375924/?format=api",
    "text_counter": 58,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Endebess, UDA",
    "speaker_title": "Hon. (Dr) Robert Pukose",
    "speaker": null,
    "content": "Wazee hao hushughulikia mambo mengi kule vijijini. Kabla mkutano wowote uanze, wazee wa Nyumba Kumi huwa wanaulizwa waeleze kinachoendelea vijijini mwao. Mambo ya security yetu inaanza na wazee wa Nyumba Kumi na wazee wa vijiji. Wazee hao wanafanya kazi muhimu. Kwa sababu hiyo, naunga mkono Mswada huu ambao umeletwa na Mhe. Malulu Injendi ili tuunde sheria ya kuwatambua kirasmi, kuwapa marupurupu na kutambua kazi wanayofanya. Hapo awali, wazee wa vijiji walikuwa wanaitwa wakati kuna mkasa. Walipokuwa wanafanya kazi ile, walikuwa wanalipwa kwa kuku, mbuzi au kondoo. Muda unapozidi kusonga, unapata kuwa malipo ya kuku hayawezi kuwasaidia kuwasomesha watoto wao na kujikimu kimaisha. Kwa hivyo, ni vizuri tutafute namna ya kuwalipa. Serikali tofauti zimezungumzia mambo ya kuwalipa wazee wa vijiji lakini hakuna ile ambayo imechukua hatua ya kuunda sheria. Kwa hivyo, ni vizuri kwetu kuunda sheria ili tuwatambue. Ni muhimu tuwe na national co-ordination team ambayo itawatambua wazee wa vijiji katika sehemu tofauti na qualifications zao ndiyo waweze kuheshimika miongoni mwa wanavijiji wote. Wazee wa vijiji wana kazi nyingi kama vile kupeana vitambulisho. Lazima wajue kuwa yule kijana anayetaka kitambulisho ni mtoto wa fulani. Wapenzi wa ndoa wanapopigana, kesi hizo huenda kwa wazee wa vijiji ili wazitatue. Nikiwa nyumbani Jumapili iliyopita, mzee mmoja kutoka kijiji cha Chepkirot anayeitwa Mzee Kambala alikuja kuniambia kuwa uhalifu katika kijiji chake umepungua kwa sababu ameshirikiana vizuri na chief, assistant chief, Deputy County Commissioner (DCC) na"
}