GET /api/v0.1/hansard/entries/1375944/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1375944,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1375944/?format=api",
    "text_counter": 78,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lungalunga, UDM",
    "speaker_title": "Mhe. Chiforomodo Mangale",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Kwanza, naunga mkono kwamba wale wazee wa vijiji waweze kulipwa mshahara. Hii ni kwa sababu hao ndio sura ya Serikali pale nyanjani. Pili, wanafanya kazi muhimu ya kuhakikisha kwamba wanalinda usalama. Tatu, hao wazee wa vijiji wanaleta uwiano kati ya Serikali na wananchi pale nyanjani. Wao huwahamasisha wananchi kuhusu miradi yote ya Serikai ikiwemo, chanjo, na miradi mingine muhimu ambayo inawaathiri moja kwa moja na kutoa mwelekeo. Naomba Mswada huu upitishwe haraka, ili wazee wetu wa vijiji waweze kulipwa mshahara wala si kiinua mgongo. Hii ni kwa sababu majukumu wanayoyafanya pale nyanjani ni muhimu sana. Tumechelewa kwa sababu Mswada kama huu huja kila wakati lakini haukamiliki..."
}