GET /api/v0.1/hansard/entries/1375998/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1375998,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1375998/?format=api",
"text_counter": 132,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa Kaunti, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Tunajua kuwa watoto wetu wengi wametoka katika vyuo vikuu, wamesomea taasisi tofauti tofauti, lakini nafasi za kazi mpaka sasa zimekuwa haba. Wakati ule wa Corona, watu wengi sana walifutwa kazi, na nafasi za kazi zikawa haba kwa sababu watu wengi pia walifunga biashara zao. Ili kuwaingiza watoto wetu katika nafasi za kazi, lazima nasi tutoe nafasi. Ukishahudumu katika Serikali na umefikia miaka 60, hiyo ni dhahiri kuwa nawe pia uweze kupisha watu wengine waweze kuchukua nafasi hiyo."
}