GET /api/v0.1/hansard/entries/1375999/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1375999,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1375999/?format=api",
    "text_counter": 133,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa Kaunti, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Ila tu ningependa kuongezea kuwa hata ukistaafu na miaka 60, pia hao waweze kuangaliwa. Tunapata wafanyikazi wengi wa Serikali wamestaafu, na mpaka sasa, marupurupu yao ama pesa zao za baada ya kustaafu hawajapata. Wengi wanalia na wanaishi maisha duni. Kwa mfano, kuna watu ambao wamestaafu katika shirika la Kenya Railways . Juzi wamenituma kwa sababu mpaka sasa hawapati marupurupu yao. Naomba tuweze kuangalia hao watu wazima ambao wanastaafu. Licha ya kuwa wanataka kutoa nafasi kwa watoto wetu, lakini nao pia ni Wakenya; waweze kuangaliwa vizuri. Tuhakikishe kuwa marupurupu ya wafanyikazi wanaostaafu wanapewa kwa wakati muafaka ndio nao pia waweze kuishi vyema."
}