GET /api/v0.1/hansard/entries/1376000/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1376000,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376000/?format=api",
"text_counter": 134,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa Kaunti, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Nimeona pia amezungumzia watu ambao wanafanya kazi kwa kujishikilia. Juzi nimekuwa Mombasa katika taasisi ya maji, nikagundua kuwa yule Mkurugenzi Mkuu ambaye anahusika pale ameshikilia kwa miaka miwili na nusu. Hajaweza kuandikwa rasmi. Hii inatamausha sana. Watu wanashikilia nafasi za kazi kwa muda mrefu bila kuandikwa kwenye nafasi zile. Ni dhahiri kuwa hata kuna waalimu ambao wamekuwa wakisomesha kama hali ya kujitolea kwa muda mrefu sana. Kuna madaktari kwenye mkataba ambao wanajitolea kutibu wagonjwa. Muda wa kuandika kazi ukifika, tungependa madaktari hao waandikwe. Isipite muda ambao umewekwa katika sheria. Tunapowatetea wafanyikazi, tukitafuta nafasi za kazi kwa vijana wetu, ni muhimu tuangalie pia makampuni yalioajiri watoto wetu kazi. Kwa mfano, juzi kumekuwa na mgomo Mombasa, na ilitamausha sana. Mgomo huo ulikuwa wa kampuni ya Export Processing Zone (EPZ), na nilijaribu kuingilia kati. Ningependa Kamati ya Leba ichunguze jambo hili. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}