GET /api/v0.1/hansard/entries/1376001/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1376001,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376001/?format=api",
    "text_counter": 135,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa Kaunti, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Watoto wetu wanaajiriwa kwa contract ya mwezi moja, ilhali wamekaa pale miaka kumi. Hii ni dhuluma kwa wafanyikazi wa Kenya na watoto wetu. Naomba Kamati ya Leba ifuatilie jambo hili na ichunguze sababu ya watoto kuandikwa kwa mwezi moja. Katika kampuni hiyo ya EPZ, kazi ni ngumu sana. Wanaanza saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa nne ya usiku. Mwezi moja unapoisha, wafanyikazi hao wanaambiwa warudi tena wajiandikishe upya, ilhali mtu amekaa pale miaka 10. Tunafaa kuangalia hali ya wafanyikazi katika taifa hili. Mhe. Spika wa Muda, ni ukweli kwamba tunataka watoto wetu wapate ajira ili taifa hili liweze kujengeka kwa ubora, lakini ni muhimu pia tuhakikishe kuwa wafanyikazi wana furaha. Ni muhimu waruhusiwe kujiunga na mashirika ambayo yameruhusiwa katika Katiba. Hii ni kwa sababu wengine wanapojiunga na mashirika haya, wanafutwa kazi. Hao ni watoto wetu na ni lazima tuzungumzie mambo haya Bungeni. Nitapeleka petition yangu kutoka kwa wafanyikazi wa EPZ Mombasa kwa Kamati ya Leba. Ni muhimu kwa mameneja na wakurugenzi wa EPZ kuitwa ili tujue kwa nini watoto wetu wanafanya kazi ngumu na kulipwa Ksh15,000 kama mfanyikazi wa nyumba. Watoto wetu wanarauka saa kumi na mbili asubuhi na kutoka saa nne ya usiku. Hawana hata mapumziko na wamepewa target ."
}