GET /api/v0.1/hansard/entries/1376002/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1376002,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376002/?format=api",
"text_counter": 136,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa Kaunti, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Ni muhimu tuangalie nafasi za wafanyikazi kupitia wazee wanaostaafu ili watoto wetu wapate kazi. Ni muhimu pia tuangalie mazingira yao ya kazi. Je, haki zao za kimsingi zinaangaliwa? Je, wanapata marupurupu yao kwa wakati? Je, mambo ya waliostaafu yanaangaliwa vizuri? Kwa hivyo, mimi kama Mama Mombasa, ningependa kuunga mkono. Ningependa pia nimpongeze Mheshimiwa aliyeleta marekebisho haya. Ni jambo ambalo limenigusa sana kwa sababu tunajua asilimia 51 ya vijana wetu hawana ajira. Hawa ndio wanajiingiza katika mambo ya mihadarati na pombe. Hivi majuzi, Naibu wa Rais amejaribu kupigana na mambo ya pombe. Watoto wanaingia kwenye pombe kwa sababu wamekaa tu bila kazi ya kufanya, ilhali wazee bado wako kazini. Hatukatai wazee kuwa kazini, lakini ikifika wakati wa kuondoka, basi wapewe nafasi ya kuondoka kwa heshima. Waangaliwe kule nyumbani watakapokaa, wapewe marupurupu yao, na afya yao kuangaliwa. Hii itahakikisha kuwa vijana wetu wanapata nafasi za kazi."
}