GET /api/v0.1/hansard/entries/1376276/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1376276,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376276/?format=api",
    "text_counter": 161,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "mazungumzo na pande zote mbili za kisiasa kukubaliana kwamba tuwe na tume ya uchaguzi ambayo wakenya wote wanaiunga mkono. Kulikuwa pia na mazungumzo mwaka wa 2008 baada ya Kenya kufanya uchaguzi mwaka wa 2007. Mambo hayakuwa sawa na wakenya wakakubaliana kwamba ni vyema wakutane ili wazungumze. Mwaka wa 2018 wakati wa handshake, aliyekuwa Rais, Uhuru Kenyatta, alikutana na Kiongozi wa Upinzani, Raila Amollo Odinga na kukawa na Building Bridges Initiatives (BBI). Ilionekana kwamba ikiwa Kenya tutaendelea mbele--- Kuna watu wanafinyika bila amani. Ingawa hawakufikia mwisho katika mazungumzo yale ya BBI kwa sababu korti ilitoa mwelekeo kwamba Katiba haikufuatwa vilivyo, mambo kadhaa wa kadhaa yalijitokeza iliyosababisha kubadilishwa kwa Katiba. Bw. Spika, hivi tena mwaka wa 2022, tulifanya uchaguzi na kukawa na kutoelewana katika matokeo ya uchaguzi. Tukafikia kwamba ni vyema pande mbili za kisiasa zikutane ili kufanya mazungumzo. Hii ndio Ripoti tunayojadili inayoitwa NADCOReport . Tuko na fursa nzuri ya kupeleka Kenya mbele na kufanya mazungumzo ambayo yatapeleka Kenya mbele katika mfumo huu wa vyama vingi vya kisiasa. Kwa kizungu sasa hivi tuko katika Constitutional moment . Wakati wa kupitisha Katiba ya 2010, tulisema kwamba kuna vipengee ambavyo ni vizuri na vingine ambavyo ni vibaya, ni kama asilimia 20. Kukawa na maelewano kwamba tupitishe Katiba hii ila ifike wakati wa kuiangalia tena. Kamati hii ilifanya kazi nzuri sana. Wakati wa kufanya kazi yake, kulikuwa na uhusishaji wa wananchi na maswala mengi yaliibuka. Katika mapendekezo ya Kamati ya"
}