GET /api/v0.1/hansard/entries/1376280/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1376280,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376280/?format=api",
"text_counter": 165,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "na pesa ya oversight ya maseneta. Maendeleo mengi yamefanyika katika magatuzi yetu kupitia hazina ya maeneo Bunge na ile ya NGAAF. Pia naunga mkono kuweka katika Katiba pesa ya oversight ya Seneti kwa sababu tayari kama maseneta, tuko mashinani na tunafanya uangalizi ya kutosha kuhakikisha kwamba pesa inayoenda kwa magatuzi inayotumika na magavana imetumika vizuri ili wananchi wetu wapate huduma inayofaa. Mheshimiwa Spika, kuna mambo ya mipaka. Ripoti inasema kwamba kuundwe kamati au Bunge iunde sheria ya kuangalia kwamba mipaka imeangaziwa. Kuna wasemaji wengi kama vile Sen. Chimera na Seneta wa Makueni waliongea kuhusu mambo ya mipaka. Hili ni swala sugu sana Kenya. Katika hili Seneti, nimeleta haya maswala ya mipaka kati ya Kwale na Taita Taveta na pia Taita Taveta na Makueni. Tukienda katika sehemu za Isiolo na Meru,"
}