GET /api/v0.1/hansard/entries/1376354/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1376354,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376354/?format=api",
"text_counter": 239,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "na County Assemblies Fund (CAF ) na Senate Oversight Fund . Vile, naunga mkono ofisi ya Kiongozi wa Upinzani na mapendekezo walioileta katika tume hii ya uchaguzi. Ni kinaya kwa sababu mambo waliojadili yangejadiliwa katika Bunge hili bila kuupoteza muda. Msingi tunaouweka katika nchi hii wa kusema ni lazima kuwe na vurugu, fitima na hali isiyo hali katika nchi yetu ili tupatane kujadili mambo haya inavunja moyo sana. Kwa mfano; mapendekezo haya yote yangeweze kutolewa kwa Kamati husika za Bunge. Waliokuwa wanaongoza Kamati hii ya majadiliano ni watu walio Bunge hili. Waliosema kuwa maoni hayo yote yangejadiliwa katika Bunge hili waligonga ndipo. Tukiuweka msingi kama huu eti kila wakati ni mvutano kama ule wa 1997, Inter-PartiesParliamentary Group (IPPG) reforms, kulikuwa na mvutano na ndio maana watu waliketi chini kuzungmza. Ijapokuwa nawapongeza viongozi wale kwa kupata nafasi ya kuketi chini, tumekuwa tunaketi hapa na Kiongozi wa Waliowengi, Sen. Cheruiyot, pamoja na Seneta wa Kaunti ya Nyamira, Sen. Omogeni. Wangeketi na kuongea kuhusu jambo hili. Mambo haya yakiwekwa katika kumbukumbu itaonekana kuwa tulikuwa hatuelewei mambo tuliyopaswa kufanya. Mapendekezo ambayo wameleta hapa kwenye ripoti, tungeyazindua katika Bunge hili na kuibadilisha Katiba. Naunga mkono nikijua kuwa hakuna siku hata moja hatujaongea na Sen. Oketch Gicheru, aliye upande wa upinzani na mimi upande wa Serikali. Tulikuwa tukiiongea kwa utulivu tulipopatana kwenye Kamati tunapokutana. Maneno ambayo yanasemwa kuwa viongozi wanapatana kwa sababu ya kuleta utulivu basi ni kinaya kwa sababu Sen. Cheruiyot anaongea na Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Mheshimiwa Opiyo Wandayi. Ni vizuri tuzichunge rasilimali zetu. Baadala ya sisi tuliochaguliwa kuchukua fursa na majukumu tuliyopewa na kufanya tunayopaswa, wengi wanasema kuwa walienda kujadiliana kuhusu gharama ya maisha. Utaongea aje kuhusu gharama ya maisha ilhali hayo mambo yalikuwa yamezingatiwa vizuri na Serikali. Serikaili ilikuwa imeweka misingi dhabiti. Tayari mbolea ilikuwa imepunguzwa bei pia. Gunia za mahindi ambazo zimevunwa kwa sababu ya mbolea iliyotolewa ni nyingi. Tunaweza kusema na kufanya mengi ili kupongeza Kamati hii. Lakini, nikiyaangalia mapendekezo hayo katika riporti hii ya kurasa 500, nina uhakika tungefanya mambo haya yote katika Bunge hili. Tunawakosea Wakenya heshima na shukrani kwa sababu walituchagua kufanya kazi hii. Badala ya ndugu zetu, Sen. Cheruiyot na Sen. Omogeni kuifanya kazi hii hapa, moja kwa moja, kiguu na njia wanaenda kuifanyia Bomas of Kenya . Ni swala linalovunja moyo na sio kwangu tu lakini kwa Wakenya wote. Nawapongeza kwa kufanya kazi nzuri. Lakini, wangeifanyia katika Bunge ili wachunga mali ya Wakenya. Swala ambalo lingekuwa bora zaidi. Kusonga mbele, msingi tunaoweka si mzuri na unavunja moyo wangu kwa Wakenya wote."
}