GET /api/v0.1/hansard/entries/1376358/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1376358,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376358/?format=api",
    "text_counter": 243,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuunga mkono ripoti ya Kamati ya uwiano ambayo iliwasilishwa na Kiongozi wa Wengi katika Bunge hili. Kwanza, natoa pongezi kwa viongozi wawili wakuu ambao walikubaliana kuwe na Kamati hii. Vile vile, wanakamati wote waliofanya kazi pamoja na watumishi wao kuhakikisha kuwa wameitoa ripoti inayokubalika. Najiunga na katibu wa chama chetu cha Orange Democratic Movement (ODM). Hata kama Ripoti hii ina mambo mengi ambayo yamezungumziwa, kuna mambo msingi ambayo hayakutajwa na kuzungumziwa kwa ufasaha. Moja wapo ikiwa ni kuongezeka kwa bei ya bidhaa muhimu katika nchi yetu. Yani gharama ya maisha imeongezeka maradufu kiasi ambacho wengi katika nchi ya Kenya hawawezi kuandaa mkate wala ugali katika meza zao kila siku. Hilo ni jambo muhimu sana. Kuongezeka kwa gharama ya miasha kuna sababisha watu kukosa namna ya kujikimu kimaisha. Wanafunzi wanakosa kwenda shule na wagonjwa wanakosa matibabu na hayo yote yanasababishwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa muhimu na maisha kwa jumla. Kwa mfano, kuongezeka kwa gharama ya Value Added Tax (VAT) ya mafuta. Swala hili lilikua hapo awali, 2018 na 2019. Serikali iliyokuwa wakati ule ili leta mswada katika Bunge la Kitaifa na ika punguzwa kutoka asilimia 16 hadi Asilimia 8. Hivyo ilisababisha kupunguka pakubwa kwa bei za bidhaa muhimu kama mafuta na zinginezo. Bi. Spika wa Muda, tukiangalia katika magazeti yetu kila siku kuna ripoti kadha wa kadha ambazo zinaonyesha ubadhirifu wa pesa za umma katika nchi yetu. Leo utasikia kuna millioni 600 za kurekebisha nyumba ya Naibu wa Rais. Hizi ni pesa za umma ambazo zinavujwa na kutumika kwa hali ambayo isiyo ya kisawasawa. Upande mwingine, wale walala hoi wanaendelea kupata shida ya kusomesha watoto wao. Watoto wengi wanakosa kusoma na baadaye wanakuwa majambazi na hali yao ya maisha inabadilika. Wenzetu wa upande ule mwingine wamesema kuwa kulikuwa na vurugu kabla ya Kamati hii na wale ambao mali yao iliharibiwa walipwe fidia. Watu wengi walipoteza maisha yao. Wengine walipigwa risasi na kuuliwa na vikosi vya usalama. Kiongozi wa Walio Wachache alishikwa akitoka hapa Bunge akienda nyumbani kwake. Kushikwa kwake kuliwapa furaha wanadada wengi. Baadhi ya Maseneta katika Bunge hili waliona raha walipomuona Sen. Madzayo ametiwa mbaroni na hali ambayo ilionyesha ni mtu wa kisawasawa."
}