GET /api/v0.1/hansard/entries/1376360/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1376360,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376360/?format=api",
    "text_counter": 245,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Mojawapo wa vipengee muhimu vya hii ripoti ni suala la Bunge kuangalia gharama ya maisha. Kwenye mchakato wa kutengeneza bajeti ya mwaka 2024/2025, gharama ya maisha lazima ipunguzwe. Suala la pili ambalo ningependa kuliguzia ni kuongezeka kwa akina mama kwenye uongozi wa nchi. Hili ni suala ambalo limekuwa donda sugu. Bunge lililopita, lilijaribu mara tatu kupitisha Mswada huu lakini haukupita. Nakubaliana na Kamati kwamba lazima watu wakae chini kama Bunge kuhakikisha kwamba suala hili linatekelezwa ili watoto wetu wa kike; dada zetu wapate fursa ya kuingia katika uongozi. Tunapoelekea itakuwa ni ngumu zaidi kwa kina dada kuingia katika uongozi wa kuchaguliwa. Kila siku wale ambao wanahusika kama viongozi wa vyama ama wale ambao wanasimamia vikundi hivi wanatumia mbinu ambazo hazifai kikatiba kuzuia wasichana kupata uongozi. Jambo la mwisho ambalo ningependa kuligusia ni kuhusu hazina ambazo ziko. Kwa mfano, hazina ya National Government Constituencies Development Fund (NG-CDF), ambayo imesaidia pakubwa kupeleka maendeleo mashinani. Tumekubali hapa kwamba hazina ya Seneti ya oversight imefanya kazi kubwa muda mchache tangu ipitishwe. Tungependa Ward Fund (WF) iwepo ili kila wardi iweze kupata maendeleo kutoka kwa serikali za kaunti zetu. Baadhi ya wadi hazipati maendeleo kwa sababu magavana hawaelewani na wabunge wa Bunge za kaunti. Kila wadi iwe na pesa zake kuhakikisha kwamba maendeleo yanafika pembe zote za wadi zetu. Tunakubaliana kwamba ipo haja kuangalia kwa haraka masuala ya mipaka ya maeneo Bunge na vilevile wadi. Hili ni swala la kikatiba na lingekuwa limeshughulikiwa kabla ya mwaka 2022, lakini halikufanyika kwa sababu za kiserikali na kifedha. Ni lazima hili jambo lifanyike ili maeneo ambayo yanastahili kupata maeneo zaidi ya ubunge yaweze kuyapata ili wananchi waweze kupata uwakilishi wa uhakika katika mabunge ya kaunti na vilevile Bunge la Kitaifa. Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii."
}