GET /api/v0.1/hansard/entries/1376434/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1376434,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376434/?format=api",
    "text_counter": 319,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii adhimu ili nami nitoe mchango wangu. Kwanza, ningependa kutoa heko kwa viongozi wetu Sen. Omogeni na Kiongozi wa Wengi, Sen. Cheruiyot, kwa kuweka kando tofauti zao za vyama vya kisiasa na kuweka taifa letu mbele. Kauli yangu ya kwanza ni kusema kwamba ripoti hii iko na kinaya kikubwa. Ni sawa na kusema kwamba ashakum si matusi lakini ripoti hii inaashiria tufunike kombe ile mwanaharamu apite. Nimetoa kauli hii kwa sababu wakati wowote tunapopiga kura za kitaifa, kuna mshindi na kuna anayeshindwa. Imetokea kwamba yule anayeshindwa kila wakati huregelea kukataa matokeo ya ushindi ule, basi tunajikuta katika hali hii."
}