GET /api/v0.1/hansard/entries/1376436/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1376436,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376436/?format=api",
    "text_counter": 321,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mimi ni kiongozi wa kizazi kipya; kiongozi mchanga katika taifa hili la Kenya. Ikiwa ripoti hii ya NADCO haitaleta suluhu kwa matukio ya kila muda, basi tutakuwa katika hali ya athari kama jamii. Niweze kuzungumzia maswala ya mapendekezo ya kikatiba ambayo yatafanyiwa marekebisho. Swala la kwanza ni lile linaanganzia mipaka na uhakiki wake. Kipengele 189 cha Katiba yetu, kinazungumzia review of boundaries . Kwa vile natoka katika Gatuzi la Mombasa, mara kwa mara, tumesikia kwamba kuna gatuzi zinaweza kuondolewa ili magatuzi mengine yaongezwe. Mimi kama mwakilishi wa eneo la Mombasa, nigependekeza ya kwamba, maeneo Bunge ya Kisauni na Likoni yagawanywe mara mbili. Hii ni kwa sababu kuna sehemu ambazo hazifikiwa na mfuko wa National Government Consitutencies Development Fund (NG-CDF) kwa sababu ya wingi wa watu wanao patikana katika maeneo bunge hayo. Bi. Spika wa Muda, pili, niwaregeshe Wakenya nyuma ili waweze kujua ni kwa nini Kamati hii ilibuniwa. Kulikuwa na hali ya sitofahamu kubwa. Kulikwa na maandamano na masufuria yaliwekwa kwenye vichwa. Ilisemekana ya kwamba ni kwa ajili ya hali ngumu ya uchumi ndiposa watu waweze kukaa chini na kuja na mwafaka wa kupeleka taifa letu mbele. Lakini, kitu kinachonishangaza ni kwamba, Dola imeweza kushukishwa, kustawishwa na kuimarishwa bila ya kuwa miongoni mwa agenda zilizokuwa katika ripoti hii ya NADCO. Kisengera nyuma chingine ambacho nimekiona katika ripoti hii ni kwamba lile zungumzo ambalo linatushika sisi kama akina mama katika taifa hili la Kenya, liliwekwa pembeni. Ngumzo la jinsia ya thuluthi zisizo zidi mbili kuwa katika taasisi zote za Serikali. Bi. Spika wa Muda, panapo tokea sitofahamu katika taifa la Kenya, pande zote mbili za uongozi husema kwamba waliomo hatarini zaidi ni watoto na akina mama. Nadhani unakubaliana na mimi. Lakini, iweje leo Kamati imekaa na wale wahusika wakuu ambao ndio wengi katika taifa la Kenya, vijana na akina mama, hoja zao kuwekwa kando. Nakashifu na na kulaani vikali, yule aliyependekeza pendekezo kama hilo na kusema kwamba, sisi kama akina mama, tunaweza kuwezesha mjadala huo tena. Hili jambo linafanyika wakati ambao kinara wa upinzani na Rais wa Taifa la Kenya wamekubaliana kuwa na gumzo kuhusu waswala mengi. Tatizo la theluthi mbili za jinsia ni tatizo la kisiasa. Hawa vinara wawili wamekubaliana kwamba lizungumziwe. Halafu mtu anakaa na fikra zake na bila hata kuhusisha viongozi wa kike katika hili taifa kuanzisha swala hili. Hapo, wametudhulumu sisi akina mama, haswa viongozi ambao tuko hapa kwa sababu ya jinsia yetu ya kutetea maswala ya jinsia ya mtoto wa kike katika taifa hili. Bi. Spika wa Muda, naomba huyo mtu ajitokeze, pamoja na wale waliokwenda katika Kamati hiyo na wawaombe msamaha wanawake na viongozi katika taifa la Kenya. Hii ni kwa sababu wameturegesha tena kuanzia alifu moja kwa ujiti. Naipongeza Kamati hii kwa kuweza kusajili rasmi ofisi ya mpinzani katika taifa la Kenya. Hiyo itaashiria kuwezeshwa, kudhibitishwa na kuimarishwa kwa upinzani ili demokrasia iweze kunawiri katika taifa letu la Kenya."
}