GET /api/v0.1/hansard/entries/1376453/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1376453,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376453/?format=api",
    "text_counter": 338,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bi Spika wa Muda, nikiendelea ningependa wawakilishi wetu wa wadi wapewe mfuko ambao utawawezesha kufanya oversight role zao kama ambavyo ripoti ya NADCO imeweza kutupa sisi kama Maseneta. Kwa sababu Kiongozi wa Wengi yuko hapa, hata sisi kama wawakilishi wa jinsia katika Bunge hili, tuweze kuwezeshwa kufanya oversight ya maswala ya kijinsia kule nje. Hii ni kwa sababu hatuko hapa kusindikiza Maseneta waliochaguliwa. Tuko hapa kwa sababu sisi pia tumetwikwa majukumu na Katiba ya Kenya ili kuwakilisha na kutunga sheria na kusimamia rasilimali na fedha zote za Wakenya wote."
}