GET /api/v0.1/hansard/entries/1378264/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1378264,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378264/?format=api",
    "text_counter": 1724,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Magarini, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante, Mheshimiwa Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi niongeze sauti yangu kwenye mjadala huu. Kwanza, ningependa kuwapongeza wahusika wakuu kwa kuona ni bora kuileta nchi yetu iwe kitu kimoja kwa njia ya kuanzisha mchakato huu. Ninaiunga mkono taarifa ya NADCO, haswa kile kipengee cha kuweza kupata theluthi moja ya Wabunge kuwa wa jinsia ya kiume au kike. Ikizingatiwa idadi ya wanaochaguliwa, ningependekeza hivi: ile tofauti iliyopo baada ya uchaguzi ambayo inahitajika kujaza lile pengo ijazwe theluthi moja ya jinsia kwa kugawiwa vyama vinavyowakilishwa bungeni . Tukifanya hivyo, tutaweza kujaza pengo la Wabunge wa jinsia hiyo ambayo ina upungufu. Tutakuwa tumetatua suala hilo la theluthi moja ya jinsia. La sivyo, itatuchukua miaka na mikaka kuweza kupata suhulu ya jambo hili. Pia, ninawapongeza wanakamati kwa kuweka NG-CDF katika Katiba yetu. Ni muhimu pia kuwa na hazina ya kata. Hazina hiyo itasaidia pakubwa kusuluhisha mvutano ambao huonekana kati ya Magavana na wawakilishi wa wadi. Hata hivyo, hazina hiyo haifai kuwekwa bila mpangilio. Hazina ya NG-CDF ina mpangilio na inasimamia vitengo."
}