GET /api/v0.1/hansard/entries/1378630/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1378630,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378630/?format=api",
    "text_counter": 286,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kinango, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nitoe maoni yangu na kuiunga mkono Hoja hii iliyo mbele yetu. Tunapozungumzia Ripoti hii ya ukaguzi wa hesabu, ni muhimu tujifahamishe kuwa Bunge hili hutenga pesa nyingi sana na kuzipatia wizara tofauti ili pesa hizo zitumike kuwasaidia wananchi ama kuleta maendeleo katika nchi yetu. Mara kwa mara, miaka nenda miaka rudi, imekuwa desturi kuwa tunazipokea ripoti hizi lakini matokeo yake mara nyingi sio ya kusaidia nchi hii kwa sababu pesa nyingi hupotea na wakati mwingine tunashindwa kujua jinsi tutakavyoziokoa. Hili ni jambo la kusikitisha kwa sababu tunaambiwa kila siku kuwa pesa zitapatikana. Kuna pesa zinazopotea kila mwaka. Sijui tutatumia lugha gani ili tusahihishe mambo kiasi cha kuwa tuiokoe nchi hii kutokana na watu ambao lengo lao kubwa ni kutafuta kazi ili kujinufaisha wao wenyewe. Mbali na kuwa Ripoti hii inawasilishwa hapa bungeni, kuna haja ya kubadilisha mtindo. Kwa mfano, siku ambayo Ripoti ya Mkaguzi-Mkuu huwasilishwa katika nchi ndogo ya Zanzibar, huwa ni public holiday . Wakati Mkaguzi-Mkuu anapokuja kuisoma Ripoti hiyo, kila atakayehusishwa na ufisadi huwa anakabidhiwa kwa mkuu wa polisi ili awe mgeni wake na kufahamishwa mashtaka atakayojibu. Akishindwa kujitetea, atakuwa mgeni wa polisi ili tulinde haki zetu. Lakini hapa Kenya, tumekuwa tukipokea Ripoti hizi na baada ya kuzijadili na kuzipitisha, hakuna hatua yoyote inayochukuliwa. Ni jukumu letu kama Wabunge kupata hatua mwafaka ili Ripoti hizi zinapopitishwa, kuwe na nafasi ya kuzisukuma kwa vile vitengo vinavyohusika na maswala ya ufujaji wa pesa ili tuhakikishe kuwa sheria inawaandama wafisadi. Pia, tuhakikishe kuwa baada ya kupitisha Ripoti hiyo na kuipeleka kwa vitengo vya upelelezi kama tume ya Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) ama Directorate ofCriminal Investigations (DCI), tupate kujua hatua ambazo wamechukua na matokeo yake. Bila ya hayo, itakuwa kazi bure. Tukumbuke kuwa pesa hizi zinatoka kwa kodi ya wananchi. Wananchi hao wanategemea Nyumba hili na viongozi walio hapa kuhakikisha kuwa tunalinda mali yao. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}