GET /api/v0.1/hansard/entries/1378631/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1378631,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378631/?format=api",
    "text_counter": 287,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kinango, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
    "speaker": null,
    "content": "Baadhi ya wenzetu huzunguka katika wizara tofauti tofauti ili kukagua jinsi pesa zetu zinavyotumika. Juzi nilisikitishwa kujua kuwa Kamati moja ya Bunge ilienda katika institution fulani na kupata kuwa pesa zilizokusudiwa kutumika kwa mradi fulani ni Ksh90 milioni na zimeongezeka kuwa Ksh300 milioni. Kama hali hii itaendelea kwa namna hii, itakuwa ni kama tunawatungia budget wale ambao hawatosheki na kile wanachokula na wanataka pia cha kuweka. Bibilia inatuambia: ‘Itanifaidi nini kuupata ulimwengu wote kisha maisha yangu yawe hatarini?’ Watu hawa wamesahau kuwa kuna Mungu na watu huishi hapa duniani na kuondoka. Nyumba hii imekuwa na Waheshimiwa waliokuwa wazungumzaji wazuri lakini mwishowe waliondoka. Kwa sababu hawajarudi, tuna matumaini kuwa walikokwenda ni kuzuri na pengine wanaona mambo mazuri. Je, mbona tunahatarisha maisha yetu kwa sababu ya kutotaka kufanya yale ambao tunastahili kufanya? Langu ni kuomba kuwa wakati mwafaka upatikane ili tuiunde sheria na kuhakikisha kuwa Mkaguzi-Mkuu wa Serikali anapofanya kazi na kuleta ripoti yake, tunaijadili, tunaipitisha na kuielekeza kwa vitengo vya upelelezi ili tujue jinsi ya kuregesha fedha zilizopotea. Leo tutatangaziwa kuwa fulani kaharibu pesa na kesho, bajeti italetwa, atapewa pesa na kufanya vile vile bila kuguswa kwa sababu pesa alizoziiba ndizo anazotumia kuendeleza na kulinda maisha aliyoyazoea. Wazungu walisema kuwa mno ni mno ama enough is enough. Kuna yule aliyesema wakati mmoja kuwa punda amechoka. Nasi tunasema kuwa ni muhimu tupate njia mbadala ya kulinda pesa zetu za kodi. Tunataka maendeleo. Kuna wale ambao wanajua tunataka maendeleo lakini kazi yao ni kusubiri na kuiba pesa. Wanauliza: “Watanifanya nini?” Kwa sababu pesa zitakapokuja, watafanya vile wanavyotaka. Tukizungumzia habari za tender, huwa kuna uhusiano fulani unaoendelea kati ya wale ambao wanazitengeneza tender documents na wale watakaofanya kazi hiyo kiasi cha kwamba anaambiwa kuwa akiufanya mradi huo na ufike kiwango fulani, alete variation document.” Jamaa huyo anajua kuwa atapata pesa ambazo si malipo ya kazi ila ni zake za kuweka mfukoni. Mwishowe, pesa zinakosekana au mradi haukamiliki. Nashindwa ni kitu gani kinachosababisha miradi inayoitwa while elephants kwa sababu miradi ilianza lakini haikamiliki. Ninavyojua sheria, kabla mradi haujakuwa tendered, ni lazima tuhakikishe kuwa kuna pesa za kutosha. Inakuwa vipi pesa ziko lakini mradi haukamiliki mpaka pesa ziongezwe? Ni lazima tujue tutaendelea kwa njia gani. Nilikuwa ninafikiria kuleta Mswada hivi karibuni, ambao utapingwa vikali lakini ni afadhali hivyo. Mtu anashikwa na kupelekwa kortini kwa sababu ametumia njia za mkato. Mwishowe, korti inatangaza kuwa mashahidi hawakuenda kortini na kesi imetupiliwa mbali. Eti vitengo vyote vya Serikali vinavyoshughulikia usalamu vinashindwa. Kwa nini shahidi hakuja mahakamani? Serikali huenda ikapata hasara lakini tusikose kumchukulia hatua yule shahidi anayejua kilichofanyika na kutoa statement ili mfisadi huyo ashtakiwe. Hivi sasa, anakaidi kwenda mahakamani kwa sababu amepewa pesa. Labda tunapaswa kuwatisha prosecutors na kuwaambia kuwa wanapotupeleka kortini na tunashinda kesi, tuna haki ya kuwashtaki kwa kutupeleka mahakamani bila ushahidi. Tutatetea hali na mali yetu kwa sababu ni lazima tujue sehemu ambazo tunapunjwa mali. Tumekuwa tukipata pesa za National Government Constituencies Development Fund ( NG-CDF) nyakati za mwisho baada ya kupeleka pesa upande mwingine tukidhania kuwa maendeleo yatapatikana, lakini pesa hizo zinaharibika kule. Tumeambiwa kuwa pesa za NG-CDF zinapaswa ziende kwa county Governments. Nimeona faida katika muda mfupi ambao nimekuwa Bungeni. Shule za upili zilikuwa sita ndani ya Kinango na za msingi zilikuwa 58. Kwa sasa nina shule 32 za upili na 187 za msingi. Kusema kweli, haki iwe ngao na mlinzi kwa sababu sisi ndio tuliopewa majukumu haya. Ni sisi tuangalie kuona kwamba tunatumia majukumu yetu vizuri ili tujue kwamba tumekamilisha kazi zetu kwa ujumla. Ahsante sana. Naunga mkono. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}