GET /api/v0.1/hansard/entries/1378633/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1378633,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378633/?format=api",
    "text_counter": 289,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ganze, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Kenneth Tungule",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nami nachukua fursa hii kujiunga na wenzangu ndani ya Bunge hili katika kuunga mkono Ripoti hii ya Mhasibu-Mkuu wa Serikali. Napongeza Kamati iliyofanya kazi hii kwa sababu imefanya kazi nzuri sana. Kusema kweli, Kenya ni nchi tajiri sana kirasilimali hata kama ina matatizo mengi. Tumepitia wakati mgumu kama taifa kwa sababu ya ufujaji wa pesa za Serikali. Mara nyingi, wale walipewa nafasi kufanyia Serikali kazi wanachukua hatua za kujinufaisha hao wenyewe. Hawaangalii vile mwananchi wa kawaida anaweza kufaidika kutokana na mapato ya Serikali. Ukiangalia miradi ambayo Serikali imeanzisha, haianzishwi kwa lengo la kumnufaisha mwananchi. Mara nyingi, inaanzishwa ili watu fulani wafaidike. Utashangaa ni kwa sababu gani miradi ya Serikali, ambayo huchukua wakati kupangwa na Serikali iliyo na watu wengi walio na masomo na ujuzi wa kutekeleza miradi, huachwa baada ya muda mfupi iwe stalledprojects ama abandoned projects. Hii ni kwa sababu hii miradi ilianzishwa bila wananchi kuwa walengwa. Miradi hii ilianzishwa ili watu wapate kick-backs zao. Baadaye, miradi inaachwa. Ukitembea nchini utapata Serikali imepoteza pesa nyingi sana. There has not been any valuefor money. Hakukuwa na faida ya ile miradi hii nchi imefanya. Ni kwa sababu miradi imeanzishwa alafu inawachwa baada ya muda mdogo. Serikali imepoteza pesa nyingi sana. Nashukuru vile hii Ripoti ya Mkaguzi-Mkuu wa Hesabu za Serikali imeleta picha kamili ya yale yanaofanyika kule mashinani."
}