GET /api/v0.1/hansard/entries/1378634/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1378634,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378634/?format=api",
"text_counter": 290,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ganze, PAA",
"speaker_title": "Hon. Kenneth Tungule",
"speaker": null,
"content": "Kama Bunge, ni lazima tuunde mikakati ya kuhakikisha kwamba mambo kama haya hayafanyiki tena kwa sababu Wakenya wanaumia. Pengine miradi hii ingewasaidia katika maisha yao ila imeishia katikati ama kuwachwa. Priorities zimebadilika. Mradi wa Serikali unawachwa na watu wanafuata shughuli nyingine. Ni kutia shime ili Bunge lihakikishe kwamba tunaweka mkazo zaidi kuhakikisha kwamba wahusika ambao walipewa jukumu na Serikali hii, kuhakikisha kwamba miradi inafanyika, wafuatiliwe pia. Ni lazima wachukuliwe hatua. Haiwezekani mradi wa Serikali uanzishwe alafu uachwe katikati bila Serikali kuchukulia hatua yoyote dhidi ya watu ambao wamefanya makosa."
}