GET /api/v0.1/hansard/entries/1378639/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1378639,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378639/?format=api",
    "text_counter": 295,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ganze, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Kenneth Tungule",
    "speaker": null,
    "content": "ila hawajalipwa. Mimi ni kuomba tu Serikali iangalie kwa sababu hawa ni Wakenya na wana haki ya kufanya biashara kama Mkenya mwingine yoyote yule. Si haki mtu afanye kazi halafu akae bila kulipwa kwa miaka mitatu au minne. Wengine wamekaa hata miaka kumi wakidai hii Serikali. Hayo ni makosa hata mbele ya Mwenyezi Mungu. Kwa Kamati inayoshughulikia mambo ya pending bills, naomba tupate suluhisho la kudumu na la haraka iwezekanavyo kwa sababu hii ni dhuluma kwa Wakenya. Kama sote tunapania uchumi wa Kenya ukue, ni lazima pia tusaidie wale wanaoshughulika kwa njia kubwa kuhakikisha uchumi wa Kenya unakua. Biashara peke yake ndiyo itakuza huu uchumi. Kama Serikali inadhulumu wanabiashara, sioni ni kwa njia gani tunaweza kusimama hapa ndani ya Bunge na tuseme uchumi wa Kenya unakua ilhali wananchi wanaumia kule kwingine. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}