GET /api/v0.1/hansard/entries/1378658/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1378658,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378658/?format=api",
    "text_counter": 314,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
    "speaker": null,
    "content": "yake ambayo imechukua karibu masaa mawili. Ametuelezea mambo ambayo yamefungua macho ya wananchi. Ingawa Mwenyekiti ametumia lugha ya Kizungu, ningependa sana kama angetumia lugha yetu ya Kiswahili, ili kila mtu kule nyumbani aelewe. Nachukua nafasi hii kupongeza Waheshimiwa wenzangu ambao wameketi nyuma yangu kwa kuchangia Ripoti hii kwa lugha ya Kiswahili. Hii ni kwa sababu Wakenya ambao wanatupigia kura ndio wanaangalia miradi ya Serikali kama shule, hospitali, ofisi ya chifu, maji ama barabara. Ufisadi unaumiza nchi na wanaoumia sana in watoto na akina mama wetu. Kwa nini nimewataja akina mama? Hii ni kwa sababu, kama hospitali inafaa kujengwe ama madawa yanatakikana na kandarasi hiyo ipatiwe mtu mfisadi, haitajengwa na madawa yatakosa. Watakaoumia sana ni watoto na wamama. Katika Katiba yetu wamama, vijana na walemavu wamepatiwa nafasi ya kupewe kandarasi za Serikali. Lakini hawapewi kwa sababu ya mawazo, vitendo na tabia za wale hupeana hizo kandarasi inaonyesha hawana haja na watu. Vijana wakipatiwa kandarasi wanaenda kwa benki kuchukua loan ndio waweze kuifanya ile kazi lakini wakimaliza, hawalipwi. Watalipa ile loan na nini? Hii imefanya vijana wetu wakose imani na kandarasi za Serikali yetu. Ndio maana umaskini uko juu, kwa sababu ya ufisadi katika taifa letu. Idadi ya watu walio wengi hapa nchini ni akina mama na vijana. Ufisadi unaumiza nchi na nina imani kwamba Serikali ya Kenya Kwanza itatatua shida hii. Hii ni kwa sababu Rais wetu amekua akisema kwamba tutamaliza ufisadi. Ninamwamini kwa sababu amejipanga na ataweka mikakati ya kuhakikisha kwamba ufisadi umemalizwa katika nchi yetu. Ufisadi ni ugonjwa mbaya sana ambao umekaa hapa nchini kwa muda mrefu sana. Mpaka wakati mwingine ukionekana hujajipanga kuiba ni kama hujui chochote na wewe ni mjinga. Ningependa kumshukuru sana Mwenyekiti, Bw. Mbadi, na wanakamati wake kwa uchunguzi ambao wamefanya. Ripoti waliyoleta hapa Bungeni ni kubwa sana na tutaisoma kwa makini. Tunataka tupekue na tuangalie kwa umakini. Na amefikisha hiyo taarifa wakati Wabunge wamekua wachache kidogo. Lakini nina wazo kwamba pengine taarifa hii itaongelewa wiki ijayo kwa sababu hii taarifa imefungua macho yetu kama viongozi na pia imefungua macho ya wananchi wa Kenya. Nataka kusema hivi kwa wananchi ambao wananisikiliza na hasa wale wa Nakuru. Kama kuna kandarasi mahali fulani, ni jukumu la mwananchi wa nchi hii kuiangalia. Hawatakikani kuomba ruhusa kwa mtu yeyote. Kama ni barabara, waulize ni nani anatengeneza na ni pesa ngapi iliwekwa. Kama ni kujenga hospitali, waulize ni nani amepatiwa kandarasi na pesa ngapi ziliwekwa. Ni jukumu la mwananchi kuangalia kila mmoja ambaye alichaguliwa kutoka juu mpaka chini. Ni kazi ya wananchi. Na hiki ndicho kitu wananchi wa Kenya hawajui. Tungependa kuchukua nafasi hii tena kuomba Serikali yetu kwamba siku za usoni, ipange vile tutaelimisha wananchi wa Kenya mambo ya Katiba kwa sababu ilipokuwa ikitengenezwa miaka kumi iliyopita, ilikuwa ikisemekana kuwa wananchi wa Kenya watafunzwa jinzi ya kutumia hiyo Katiba. Unaweza fikiria kwamba mambo yanafanyika vizuri hapo nyumbani lakini shule haijajengwa vizuri na wazazi wanaona na hawajui pia ni jukumu lao. Mambo yataharibika hapo na sisi sote tutaumia. Kwa hivyo, hii tarifa imetufungua macho. Imenifungua macho kama kiongozi kutoka Nakuru na ninapoongea sasa, ninapitisha taarifa kuwa wananchi wa Kenya wajue pia ufisadi ni ugonjwa mbaya sana na ndio umemaliza nchi yetu na ndiyo umetuumiza na wale wameumia sana ni akina mama. Mhe. Spika wa Muda, ningependa kuendelea kuongea lakini kwa sababu masaa yanayoyoma, ningependa kufikisha hapo na niseme ahsante sana."
}