GET /api/v0.1/hansard/entries/1378660/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1378660,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378660/?format=api",
"text_counter": 316,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nami nizungumzie kuhusu hii Ripoti. Mwanzo, nimpongeze Mhe. Mbadi kwa kutupatia sisi hii nafasi kusoma Ripoti na kufungua macho kama wengine wanavyosema. Ni hakika kwamba miradi mingi imeachwa bila kukamilika Kenya nzima. Kwangu Lamu Mashariki ni mojawapo. Katika eneo ninaloliwakilisha, kila kijiji kuna miradi ambayo haujakamilishwa. Inasikitisha sana kwa sababu mradi ule ulikuwa unajengwa kusaidia wananchi. Lakini ukijengwa na kuachwa katikati, basi ile sababu ya kujengwa haitapatikana. Kwangu kuna Kijiji kinaitwa Mwajumali. Sisi watu wa Lamu ya Mashariki tuko kwenye visiwa na tatizo letu kubwa huwa ni mambo ya ngome. Ngome kwa lugha ya Kimombo ni seawall . Sasa kuna vijiji vingi vina matatizo hayo. Kijiji kimoja ni Mwajumali ambapo ngome ilipewa mwanakandarasi. Mwanakandarasi nafikiri pesa aliyopewa ni kutokana na"
}