GET /api/v0.1/hansard/entries/1378662/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1378662,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378662/?format=api",
"text_counter": 318,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": null,
"content": ". Lakini mwanakandarasi alienda kujenga pahali padogo kisha akakimbia. Sasa huwa ni hasara kwa Serikali kwa sababu ya pesa ambayo imetumika. Maji bado inaingia mbele na kuvunja mpaka ambapo pesa ilitumika. Hiyo ni hasara kwa Serikali na wananchi wetu bado wanapata shida. Jambo hilo linasikitisha. Maji ikiingia, inaenda hadi kwa jiko, inabeba sufuria na inaenda nazo baharini kwa sababu mtu alipewa pesa na hakumaliza kazi. Kisha unashangaa mpaka sasa hujamwona mwanakandarasi huyo, hayuko kortini wala haujui mahali alipo. Hata ukiulizia kwa Wizara, hiyo projec t, unaambiwa haijulikani na kitu kilijengwa na dhibitisho liko kwa sababu kuna kipande nusu. Lakini itakuwa vizuri kwa Ripoti hii kuhakikisha kwamba yule ambaye alipokea pesa au kama Serikali itajenga tena, ihakikishe imejenga kwa njia ambayo itadhibiti kile kipande kidogo kilichopo ili kisiharibike. Mhe. Spika wa Muda, kijiji kingine ni Kizingitini. Huko kuna ngome lakini ngome ni nusu. Shule zinabebwa na maji kwa sababu ya mwanakandarasi au pesa iliyotolewa haikuwa kamili. Kwa hivyo, hii Ripoti ikipelekwa kwa Kamati ya Utekelezaji, ihakikishe imefuata hii miradi ambayo haikukamilishwa ili miradi yote iweze kukamilishwa."
}