GET /api/v0.1/hansard/entries/1378664/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1378664,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378664/?format=api",
    "text_counter": 320,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": null,
    "content": "Miradi ingine inafanywa kwa hadhi ambayo si sawa na jinsi ilivyo kwenye vitabu. Utasikitika kuwa pesa ya Serikali inajenga mradi na kwa miezi mitatu, huo mradi umeharibika. Kwa mfano, kwetu kuna mradi wa ngome ambao ulifanywa Mkokoni. Watu wanashangaa nazungumzia ngome sana na hawaelewi. Ngome ni seawall ambayo inazuia bahari isiende ikasomba kijiji ikaenda nayo. Kuna ngome ambayo imejengwa, na baada ya miezi mitatu, imeanguka. Inaonyesha pesa hapo zimefujwa. Kwa hivyo, hii Ripoti pia iangazie mambo kama hayo na Mwenyekiti yuko hapa afuatilie."
}