GET /api/v0.1/hansard/entries/1378665/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1378665,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378665/?format=api",
    "text_counter": 321,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Spika wa Muda, kuna tatizo lingine kwa walio kwenye mamlaka. Kama ni vinara wa kamati au wale wa ofisi za Serikali, miradi inaenda kwa walio wengi. Hilo ni tatizo kubwa. Sisi wa Lamu Mashariki, hata huu mgao wa National Government Constituencies Fund (NG- CDF), watu wakisikia hapa, Lamu Mashariki ndio inapata kidogo zaidi. Lakini utaona kuwa mtu ambaye yuko kwenye kamati, au kwenye nyadhifa za katibu ama waziri, pesa zinapelekwa sehemu zao. Ikipelekwa sehemu zao, sisi kule tunazidi kukaa nyuma."
}