GET /api/v0.1/hansard/entries/1378668/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1378668,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378668/?format=api",
"text_counter": 324,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": null,
"content": "Ukiangalia NG-CDF, ilikuwa mwanzo ikigawanywa sawa kwa sababu maeneo mengine yalikuwa yameachwa nyuma. Mwajua, kwa historia, maeneo yalikuwa yamewachwa nyuma. Ili kuyaleta yale maeneo kuwa sawa na mengine, ilikuwa imewekwa iwe sawa ili kule nako kuinuke kuwe kama maeneo Bunge mengine. Lakini utaona watu wanatukanyaga kwa kuwa hatuko wengi. Mimi ni Mbajuni pekee yangu hapa. Lakini mimi ni Mkenya. Yafaa Wakenya wengine hapa watufikirie maana hili Bunge ndilo linatengeneza bajeti na kuangalia vitabu vya akaunti. Ikiangalia, yafaa kurekebisha lakini kwa kuwa nambari zetu ni chache, lazima tuje hapa kushukuru kwa kile tunachopata kwa NG-CDF. Haki ya Mungu, hamtufanyii haki. Hii ni kwa sababu pesa za Wakenya zinatumika zaidi katika upande wa usalama. Mnatukataza kutekeleza miradi kwetu Lamu lakini pesa hizo zinakuja Lamu katika upande wa usalama. Ukosefu wa usalama haumdhuru mkaazi wa Lamu pekee yake. Magaidi wakipita Lamu wanaweza kufika Nairobi. Mngeamua kuwa kwa sababu tunapata NG-CDF kidogo, basi tusukumiwe miradi mingine. Lakini huwezi kuona mradi mkubwa kwenye Ripoti isipokuwa ile ya Lamu Port-South Sudan-Ethiopia Transport (LAPSSET) Corridor Project . Mradi wa LAPSSET ni wa Kenya nzima, si wetu pekee. Msihesabu pesa zilizotengewa LAPSSET. Watu wetu wanatatizika kule Lamu Mashariki, kwa sababu hakuna barabara wala ngome, lakini LAPSSET inahesabika kama ni ya Lamu. Mpaka sasa, haijamsaidia mkaazi yeyote wa Lamu. Kwa hivyo, kuna haja ya sisi kusukumiwa miradi mingine kama ujenzi wa barabara, ngome, maji na umeme. Mpaka sasa, hatujaunganishwa na Wakenya wengine. Tuko kivyetu. Kile kinachowaunganisha Wakenya ni barabara. Alhamdulillah tunashukuru kuwa Serikali hii imezindua barabara. Kile kinachowaunganisha Wakenya ni ile national grid . Mpaka sasa, tunatumia majenereta kule kwetu. Sijui kama Kamati hii imezingatia kuwa yale mafuta yanayotumika katika majenereta kule Lamu Mashariki yanafanya bei ya umeme iwe ghali. Laiti mngekubali kutenga Ksh300 milioni ili Lamu Mashiriki iunganishwe kwenye national grid …"
}