GET /api/v0.1/hansard/entries/1378928/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1378928,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378928/?format=api",
"text_counter": 34,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Serikali ya Kenya Kwanza ilipochukua usukani, ilituahidi kujenga mabwawa matatu upande wa juu. Kuna Bwawa la Thambana ambalo linafaa kusaidia watu wa Manyatta, Mbeere South, Mwea na Kiambeere. Vile vile, kunafaa kuwa na Bwawa la Thosi ili kusaidia watu wa Runyejes na Mbeere North. Bwala lingine ni Kamumu ambalo linafaa kusaidia watu wa Mbeere North ili kuwawezesha kufanya ukulima. Bw. Waziri, ningependa ueleze watu wa Kaunti ya Embu mipangilio ilipofikia. Wakati wa kiangazi, bwawa ambalo liko upande wa Mbeere ambalo rafiki yangu ametaja lilileta shida. Ng’ombe na mbuzi wengi walikufa kutokana na shida ya maji. Bw. Waziri, ningependa utueleze wakati gani miradi hiyo mitatu itaanzishwa ili watu wa Kaunti ya Embu waache kutaabika na waweze kufanya kilimo bora."
}