GET /api/v0.1/hansard/entries/1379056/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1379056,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1379056/?format=api",
    "text_counter": 162,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Linturi",
    "speaker_title": "The Cabinet Secretary for Agriculture and Livestock Development",
    "speaker": {
        "id": 69,
        "legal_name": "Franklin Mithika Linturi",
        "slug": "franklin-linturi"
    },
    "content": " Kama sheria za Bunge hazijabadilika, nafikiria swali lingeulizwa kwa Kiswahili lingejibiwa kwa Kiswahili. Kwa hivyo, nitajaribu kujibu hilo swali kwa lugha ya Kiswahili. Nakubaliana na Sen. Munyi Mundigi ya kwamba kilimo ni idara ambayo inaweza kubadilisha na kumaliza umaskini katika taifa letu. Nashukuru wakulima wa Kenya, haswa wale wa Mbeere na wa Kaunti ya Embu, kwa kusikia mwito wetu wa kuwaomba warudi kwa mashamba na kulima ili tuweze kumaliza janga la njaa katika taifa letu. Kwa sababu hiyo, tunajivunia wakati huu kuwa tumezalisha chakula cha kutosha tukazidi yale makisio ya miaka mingi ama ile tulikuwa tumewekelea kwa kuzalisha chakula kwa msimu wa mvua uliyopita. Maembe ni mojawapo wa mimea ile tunaangazia kwa sababu ni mmea ambao tumepata hata soko yake kule nje. Wakati nilikuwa Pakistan na Israel, tulikuwa na mipango ya vile tunaweza kuwapelekea maembe na mananasi. Wakati wa Julai mwaka uliyopita, mimi mwenyewe nili flag off ndege a kupeleka maembe na mananasi kule Israel. Maembe yanafanya vizuri kule Mbeere na hata kule Kaunti ya Makueni, ukambani. Kila kaunti inataka tuangazie mambo inayofanya. Wiki mbili zilizopita, nilikuwa katika Kaunti ya Makueni na watu huko walitoa maoni hayo. Nikiwa hapa Bungeni, nasema kuwa katika Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, tuko na project ambayo inaitwa The National Value Chain Development The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}