GET /api/v0.1/hansard/entries/1379112/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1379112,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1379112/?format=api",
    "text_counter": 218,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Siku nyingi tukienda kwa Waziri tunakuja kulalamika. Leo tutashukuru kwa sababu kuna jambo moja tuliloleta kwa Bunge la Seneti na akafanya. Tulipoandika barua kama Kamati ya Kilimo kuhusu macadamia na kuondoa marufuku ya kuyauza ambayo ina maganda, alifanya hivyo. Ilikuwa inauzwa Ksh30 kwa kilo, sasa hivi inauzwa Ksh120 kwa kilo. Mwezi ujao itafika Ksh150. Hiyo ndiyo kufanya kazi na kuwasaidia wakulima wetu. Lakini, kuna barua nyingine itakayokuja mezani kuhusu korosho kutoka kwa wenzetu wa Pwani. Ukifanya hivyo, wenzetu pia watapata natija katika uuzaji wa korosho katika eneo la Pwani. Jambo la pili, Bw. Waziri, tulipokaa kama Kamati, tulichunguza bajeti ya mwaka huu. Kilimo inatupatia kadiri ya asilimia 20 ya mapato ya nchi hii. Lakini, tuliona umepata asilimia tatu kwa bajeti. Tunajua wewe ni mfalme wa mistari. Sijui kama mistari imekupotea kidogo ukashindwa kutongoza Wizara ya Fedha kukupatia fedha zaidi. Lakini ni muhimu Wizara yako iongezewe fedha. Tutapeana barua zetu katika Bunge ili tustawishe kilimo kama uti wa mgongo wa nchi yetu na pia kuhakikisha kuna usalama wa chakula nchini. Jambo la tatu ni kero la konokono. Wakulima wa mpunga kutoka Mwea, Bunyala na Ahero wamesumbuliwa sana na konokono. Tunavyojua, Bw. Waziri, konokono hana mwendo. Ingekuwa ni panya, tungeelewa kwa sababu anakimbia. Ingekuwa nzige, tungeelewa kwa sababu anapaa. Lakini konokono hana mwendo. Hilo janga tusipoliangalia vizuri, hatutakuwa na mpunga, hasa katika eneo la Mwea. Naomba taasisi inayohusika kudhibiti wadudu waharibifu, waangalie suala hili. Ndiposa tumekualika tarehe 15 kule Mwea, uje tuketi pamoja ili tuangalie suluhisho la janga hili. Mwisho, mbolea ya ruzuku imekuwa ya maana sana. Umeitisha majina, lakini mahali nimetoka Kirinyaga, vyama vya ushirika ni 14. Kwa hivyo, mbolea ikipelekwa kwa wakulima wa kahawa katika vyama vya ushirika, wote watapata mbolea pasipo kuwa na shida. Wako na maghala yaliyo na usalama wa kuweka mbolea . The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}