GET /api/v0.1/hansard/entries/1379113/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1379113,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1379113/?format=api",
    "text_counter": 219,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Wakulima wa mpunga wako na shida ile ya mbolea. Mbolea ya mpunga ni tofauti sana. Kuna Sulphate Ammonia, kuna ile wanaita sukari na Triple Superphosphate (TSP), ambayo haitumiki katika ukulima wa mahindi. Ukienda sasa hivi, utapata wakulima wengi wako na ujumbe, lakini hawawezi kupata mbolea . Mahali unapata mbolea, unapata kuwa ujumbe unachelewa. Ningeuliza Katibu anayehusika na kilimo, aangalie hili jambo ili kuhakikisha kwamba ujumbe unafikia wakulima ifaavyo ili waweze kupata mbolea. Pia nakushukuru kwani najua kazi yako ni ngumu lakini umeimudu. Waswahili wanasema kuwa ni kazi msaragambo. Wewe ni mwenzetu, tukija na malalamishi yoyote, tafadhali tusikize. Hii ni kwa sababu tunajua majukumu yetu na kilimo imegatuliwa. Asante, Bw. Naibu Spika."
}