GET /api/v0.1/hansard/entries/1379665/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1379665,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1379665/?format=api",
"text_counter": 61,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": null,
"content": " Yes. Ahsante, Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii nichangie marekebisho ya sheria ya Tume ya Utumishi kwa Umma. Kwa muda mrefu sasa, tumeona wakurugenzi ambao wameendelea kuhudumu wakiwa hawajapewa nyadhifa au uwezo kamili katika mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na pia kwenye taasisi nyingi za serikali. Wamekuwa wakishikilia nyadhifa hizi kwa muda mrefu na hawawezi kufanya maamuzi yanayosaidia hayo mashirika. Kwa mfano, utaona mtu ameshikilia wadhifa kwa miaka miwili, mitatu au minne. Nafasi ya kazi inapotangazwa, yule ameshikilia wadhifa huo kwa miaka miwili au mitatu anatolewa na mwingine kupatiwa nafasi hiyo kwa sababu aliyeshikilia hana uwezo au ushawishi wa kisiasa. Huenda anayepewa wadhifa huo alikuwa mdogo wake kikazi. Inasikitisha kwa sababu inarudisha nyuma ile ari au azma ya mtu kujitolea kufanya kazi yake. Kuna taasisi nyingine ambazo mtu akimaliza kuhudumu miaka yake, pengine miaka 55, anaongezwa miaka miwili ili kuendelea na kazi ile. Jambo hili limenyima vijana wengi nafasi za kazi. Mtu anayefikisha umri wa miaka 55 au 60 anastahili kustaafu ili kupatia watu wengine, hasa vijana, nafasi hizo za kazi. Kama tumeamua ama sheria imepitishwa kwamba mtu atastaafu akitimu miaka 55 au 60, iwe hivyo. Hiyo itapatia mashirika yasiyo ya serikali na taasisi mbalimbali nafasi ya kufundisha watu fulani ambao watashikilia nyadhifa zile. Isiwe ni mtu mmoja tu aliye na ujuzi Kenya nzima hata asipatie wengine nafasi. Jambo hili limewadhalilisha vijana walio na shahada na hawawezi kupata nafasi kwa sababu wanaotakikana kustaafu wanaongezewa muda wa kuendelea kuhudumu. Ninaunga mkono marekebisho ya Mswada huo. Ahsante, Mhe. Naibu Spika."
}