GET /api/v0.1/hansard/entries/1379697/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1379697,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1379697/?format=api",
"text_counter": 93,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Pia, ninaunga mkono vile Mhe. alivyosema hapa kwamba matayarisho yafanywe mapema kwa sababu inachukuliwa kama kigezo ili mwingine aendelee kufanya kazi na kusema hakuna mwingine anawezakufanya taaluma yake. Ni vizuri vile ilivyosemwa kwamba kabla yule mwenye taaluma ile hajaondoka, mwingine atayarishwe achukue hiyo nafasi yake. Isiwe kiegezo cha kukosesha wengine kazi kwa kumpendelea mtu mwingine. Pia, ninaunga mkono pale anaposema wale makatibu washikilizi wasifanye zaidi ya miezi sita. Kusema kweli, tunapoteza sana kwa sababu wakikaa pale, utaona katibu amekuja kazini hata hana morali kwa sababu hajui kesho kutakuwa vipi. Katibu ajue akienda sana ni miezi sita. Aandikwe au atolewe. Kwa haya yote tunayozungumza, iwe ni kwa wale wanaopitia Tume ya Utumishi wa Umma. Nilikuwa nimeshtuka nikiona kuwa itabidi pia marubani na majaji watastaafu kwa miaka sitini. Kitu kinachoweza mfanya rubani astaafu ni afya yake. Daktari akisema huyu hafai kurusha ndege, ndio hafai. Mheshimiwa amenihakikishia kwamba haya mapendekezo ni kwa wale wanaopitia Tume ya Utumishi wa Umma. Majaji hawako kwenye huu mpango. Kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}