GET /api/v0.1/hansard/entries/1379710/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1379710,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1379710/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kinango, PAA",
    "speaker_title": "Mhe. Gonzi Rai",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nami pia ningetaka kutoa sauti yangu kuhusiana na Mswada huu ulioko mbele yetu. Mswada huu umekuja kwa wakati mwafaka. Tunapozungumzia maswala haya ya kazi, ni muhimu tufahamu kwamba lengo kubwa hasa la Mswada huu ni kuboresha morali ya wafanyikazi katika Huduma ya Umma, kwa sababu ya ule ugandamizaji ambao uko kwenye sekta hii. Kumekuwa na hatari ambazo zimekuwa zikifanyika hasa kwa watu ambao wako kwenye sehemu kame kama kule kwangu Kinango. Pengine mwalimu anastaafu na anayemshikilia anapewa nafasi ile na anakaa pale kwa muda wa karibu miaka sita. Mhe. Spika wa Muda, unapata kuwa mwalimu huyo anatosha kupewa nafasi hiyo lakini kwa sababu ya kutojua mtu wa kumsaidia, inabidi akae mahali pale miaka sita. Baadaye, mwalimu mwingine analetwa kuchukua nafasi hiyo na yeye anapewa nafasi ya naibu wa mwalimu mkuu. Hili ni jambo la kuvunja moyo sana kwa sababu unapofanya kazi, inafaa tajiri aelewe taabu na mashaka yako. Mfanyikazi anafaa kutosheka na kile anachokifanya kwa sababu ni faida kwa Serikali. Ni muhimu pia yeye ajisikie yuko kazini na anafurahia kazi yake."
}