GET /api/v0.1/hansard/entries/1379711/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1379711,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1379711/?format=api",
"text_counter": 107,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinango, PAA",
"speaker_title": "Mhe. Gonzi Rai",
"speaker": null,
"content": "Tumekuwa na machifu na wafanyikazi ambao wanafanya kazi katika sehemu kame. Kule Kinango, walimu wanapatiwa hardship allowance lakini machifu, County Commissioners, Deputy County Commissioners, Assistant County Commissioners na wafanyikazi wengine wote wa Umma walio kule hawalipwi. Tunapouliza shida hii inatokana na nini, hakuna jibu isipokuwa kuzungushwa. Mkaguzi wa Hesabu huja hapa miaka nenda, miaka rudi akitueleza kuwa mtu anastaafu lakini haondolewi katika orodha ya wafanyikazi; mwenye kumshikilia anabaki pale miaka kumi ili watu waendelee kupokea pesa za yule aliyestaafu. Wakati mwingine machifu wanapoelekea kustaafu, wanapeana notice ya likizo wakisubiri retire . Linalostaajabisha ni kwamba baada ya likizo, wanapostaafu, pensheni yao huchukua hata miaka sita kabla ya kulipwa. Wengine wanakufa kabla ya kupata pesa zao. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}