GET /api/v0.1/hansard/entries/1379712/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1379712,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1379712/?format=api",
"text_counter": 108,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinango, PAA",
"speaker_title": "Mhe. Gonzi Rai",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Spika wa Muda, ni muhimu tuwe na utaratibu maalum wa kuhakikisha kuwa mwalimu, chifu au mfanyikazi yeyote anapostaafu anapata haki yake baada ya miezi mitatu au sita. Tunawaua watu wengi. Ni jambo la kusikitisha. Mara kwa mara, tunaskia kuwa wizara fulani ina wafanyakazi gushi na wote wanalipwa mshahara, lakini aliyefanya kazi kwa kujitolea katika nchi hii anabaki akisubiri malipo yake ya uzeeni na hawezi kupata. Hili ni jambo ambalo linafaa kuangaliwa kwa undani. Ningependa kumshukuru Mheshimiwa aliyeleta Mswada huu kwa sababu anajua kitu ambacho kinahitaji kuangaliwa ili kuleta ukarabati na uwiano."
}