GET /api/v0.1/hansard/entries/1379790/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1379790,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1379790/?format=api",
    "text_counter": 186,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Msamweni, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Feisal Bader",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi nami pia niongeze sauti yangu kwa kuuchangia Mswada huu. Ningependa pia kumpongeza Mhe. Emaase kwa kuuleta Mswaada huu muhimu katika taifa letu la Kenya. Ukulima wa pamba ni sekta ambayo imetelekezwa kwa muda mrefu; kwa miaka mingi. Kama taifa, tumepoteza kiuchumi kwa muda mrefu. Kwa hivyo, ninataka kumpongeza Mhe. Emaase kwa kuuleta huu Mswaada ambao utarudisha haadhi na kuboresha ukulima wa pamba. Ukulima wa pamba haufanyiki sehemu za Magharibi tu bali pia Mkoa wa Pwani katika Kaunti za Kwale, Lamu, Kilifi na Taita Taveta. Ni masikitiko makubwa sana kwa kuwa huu muda wote, hakuna hata kinu kimoja cha kuchambua pampa katika Eneo La Pwani. Ningependa kumpongeza Mhe. Rais na Serikali ya Kenya Kwanza kwa kuwaangalia watu wa Pwani na kuhakikisha kuwa wakulima wa pamba watafaidika. Kwa muda wa wiki mbili, Mhe. Rais atakuja rasmi kuzindua kinu cha kuchambulia pamba katika Eneo Bunge ninaloliwakilisha la Msambweni, Wadi ya Kinondu. Mswada huu utalinda wakulima kutokana na wale madalali ambao wamekuwa wakinyanyasa wakulima kwa muda mrefu. Tunapoangalia katika sekta ya sukari, imeanguka minajili ya madalali. Mswada huu utasaidia pakubwa, kuwaondoa ili wakulima wafaidike. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}