GET /api/v0.1/hansard/entries/1379791/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1379791,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1379791/?format=api",
    "text_counter": 187,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Msamweni, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Feisal Bader",
    "speaker": null,
    "content": "Huu Mswada pia, umetaja ongezeko la dhamani wa pamba. Kila wakati tunaposikia ongezeko la dhamani kwa bidhaa, inamaanisha kuwa mkulima atapata faida kubwa kwa sababu gharama ya bei pia itapanda. Pili, tunaposikia ongezeko la dhamani, inamaanisha kuwa ajira itapatikana kwa vijana wetu. Hili ndilo swala ambalo tunalipatia kipao mbele kama Taifa. Sitaki kuendelea zaidi ya hapo lakini niwasihi Wabunge wenzangu kwa ujumla waunge mkono huu Mswada ili tuupitishe uwe sheria kwa haraka."
}