GET /api/v0.1/hansard/entries/1379807/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1379807,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1379807/?format=api",
"text_counter": 203,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "wameajiri zaidi ya vijana karibu 200,000. Vijana wetu wanaofanya katika hayo makampuni ya pamba wameweza kupata ajira kule. Zile mbegu za pamba unaona zinatoa sabuni, mafuta masafi, chakula cha kuku, yaani kila kitu ndani ya pamba kina thamani yake. Kwa hivyo mimi ninataka kusema kwamba hii pamba na hata bidhaa zingine ambazo ni cash crops kwetu tukifufua basi itaweza kufufua uchumi mkubwa wa Kenya na maisha yatakuwa mazuri katika Taifa letu. Tukiweza kupandisha pamba katika anga ambazo zinasifika, tutaweza pia kupandisha ya chai, nazi na pia korosho. Hizi ni bidhaa ambazo tukiziwekeza katika ukulima, mazao ya taifa hili yatakuwa mazuri na hata Wakenya watakuwa na furaha ya kulipa ushuru."
}