GET /api/v0.1/hansard/entries/1379944/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1379944,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1379944/?format=api",
    "text_counter": 124,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Kitendo kama hicho ni jambo ambalo linafaa kukemewa. Kwa hivyo, hatua inafaa kuchukuliwa. Tuna Kamati ya Usalama wa Taifa na Masuala ya Kigeni katika Seneti. Kamati hiyo inafaa kuchunguza sababu za kutokea kwa kitendo hicho na kuhakikisha kuwa waandishi wa habari au wale waliokuwa wakichukua picha pamoja na watu wengine ambao hawakuwa huko Bomet wamearifiwa. Watu kama hao lazima wapewe ulinzi wa kutosha. Kwa hivyo, Bw. Spika, ninapounga mkono Taarifa hii, ningependa kusema kuwa ni vyema Baraza la Wanahabari Nchini Kenya, ambao ni wakubwa wa waandishi wa habari, linafaa kupewa nafasi ya kuangalia kwa kina na kuhakikisha kuwa haki ya wanahabari wale imetendeka. Asante."
}